Jamii Dashibodi: Jukwaa rafiki la vijana lenye nyenzo za kujifunza, tathimini, majadiliano, rufaa na maoni kuhusu elimu na huduma za Afya ya Uzazi pamoja na VVU/UKIMWI.
Elimika: Jitathimini mwenyewe au marafiki na uboreshe uelewa, mitazamo na matendo yako juu ya masuala yanayohusu Afya ya Uzazi pamoja na VVU/UKIMWI huku ukishirikiana na marafiki, wazazi na washauri katika jamii.
Fanya maamuzi sahihi: Tumia data zilizowasilishwa kwa urahisi kwenye dashibodi zinazoelezea hali ya uelewa, mitazamo na matendo ya vijana katika jamii yako juu ya masuala yanayohusu Afya ya Uzazi pamoja na VVU/UKIMWI.
Data kuhusu Afya ya Uzazi na VVU/UKIMWI kwa Vijana
Angalia data zilizowasilishwa kwa urahisi kwenye dashibodi zinazoelezea hali ya uelewa, mitazamo na matendo ya vijana katika jamii juu ya masuala yanayohusu Afya ya Uzazi pamoja na VVU/UKIMWI.
60.75%
Uelewa
60.75% ya washiriki wa 'Jitambue challenge' wanaonyesha wana uelewa juu ya njia za kuzuia VVU/UKIMWI, Upimaji na Matibabu.
78.05%
Matendo
78.05% ya washiriki wa 'Jitambue challenge' wanaonyesha wana matendo yasio hatarishi juu ya njia za kuzuia VVU/UKIMWI, Upimaji na Matibabu.
76.17%
Mitazamo
76.17% ya washiriki wa 'Jitambue challenge' wanaonyesha wana Mitazamo chanya juu ya njia za kuzuia VVU/UKIMWI, Upimaji na Matibabu.
Jitambue App
Jitambue App ni Jukwaa rafiki linaloruhusu vijana na wazazi kujifunza, kujitathimini, kujadiliana, kupata rufaa na kutoa maoni kuhusu uelewa, matendo na mitazamo juu ya elimu na huduma za Afya ya Uzazi pamoja na VVU/UKIMWI katika jamii. Jiunge sasa.